Jilinde mwenyewe na walinde wengine kwa corona virus

 

Virusi vya corona vipo, na tunakutaka uwe mwangalifu!

Ustawi na uzima wako ndivyo vipaumbele vikuu kwetu! Jukwaa letu ni sehemu bora kabisa katika kukukutanisha na marafiki wapya. Na ingawaje tunapenda ufurahie maisha yako hapa lakini kujikinga na virusi vya korona ni jambo muhimu sana. Hivyo basi, tunashauri njia za kujikinga na virusi vya korona zikiwa ni pamoja na kunawa mikono, kubeba vitakasa mikono, kuepuka kugusa uso wako na kuhakikisha unakaa mbali na watu kwenye mijumuiko.

 

Hii ikiwa ni pamoja na kujizuia kubusiana, kukumbatiana pamoja na kushikana mikono na mpenzi wako mtarajiwa.

 

 

Ushauri kutoka Shirika la Afya Duniani, yaani WHO

(World Health Organisation) https://www.who.int/

 

Osha mikono yako mara kwa mara

Safisha mikono yako mara kwa mara kwa kutumia sabuni na maji safi yanayotiririka, au tumia vitakasa kusugulia viganja vyako.

Kwanini? Virusi ambavyo vinaweza kuwa mikononi mwako vitakufa endapo utaosha mikono kwa sabuni na maji yanayotiririka au ikiwa utatumia vitakasa mikono kusugua viganja vyako.

 

Epuka kukaribiana na watu

Hakikisha unakaa au kusimama umbali wa angalau mita 1 (yaani futi 3) kutoka alipo mtu yeyote anayekohoa au kupiga chafya.

Kwanini? Wakati mtu anapokohoa au kupiga chafya, anakuwa anasambaza vimajimaji kupitia mdomo au pua. Kama mtu huyu ana virusi vya corona, basi vimajimaji hivi pia vitakuwa na virusi. Sasa ukikaa karibu na mtu wa aina hii, hivi vimajimaji vyenye virusi vya corona vitaingia mwilini mwako kwa njia ya pua au mdomo, na hivyo kukuambukiza.

 

Jizuie kugusa macho, pua na mdomo

Kwanini? Kama tujuavyo, mikono huwa inagusa sehemu nyingi, na ikiwa sehemu hizo zina virusi vya corona, basi mikono itabeba hivyo virusi.  Mikono hii ikishakuwa na virusi basi inaweza kusafirisha virusi hivyo vya corona hadi kwenye macho yako, mdomoni au puani. Kutokea hapo, virusi vya corona vinaweza kuingia mwilini mwako na kukusababishia ugonjwa wa virusi vya corona.

Kumbuka kwamba, virusi vya corona vinaweza kuishi hata kwenye sehemu ngumu kamavile juu ya meza, kwenye kompyuta na hata simu; simu ambazo mara kwa mara huwa tunazigusa kwa mikono yetu.

 

Jifunze kutumia njia safi na salama za kupumua

Hakikisha wewe, na walio jirani yako mnafuata njia safi na salama za utoaji hewa. Hii maana yake ni kwamba, ikiwa unapiga chafya au kukohoa, basi hakikisha unaziba mdomo au pua kwa kutumia karatasi nyepesi za tishu, au kunja mkono wako kisha ukohoe au kupiga chafya kwenye kiwiko. Ukitumia tishu, basi tishu zilizotumika zitupie sehemu maalumu mara moja.

Kwanini? Vitone au vimajimaji vinavyotokana na kukohoa au kupiga chafya huwa vinasambaza virusi. Unapotumia njia salama za utoaji hewa, itakuwa unawalinda watu wa karibu dhidi ya virusi kama vile vinavyosababisha homa, mafua na virusi vya corona, yaani COVID-19.

 

Endapo una homa, unakohoa, au unapumua kwa shida, basi fanya haraka ukaonane na wataalamu wa afya

Kama hujisikii vizuri basi tulia nyumbani. Kama una homa, kikohozi, au unapata shida wakati wa kupumua, basi fanya haraka ukaonane na mtaalamu wa afya. Fuata maelekezo ya wataalamu wa afya waliopo maeneo unayoishi.

Kwanini? Wataalamu wa afya, katika ngazi ya taifa au ya mtaa watakuwa na taarifa za karibuni kabisa kuhusiana na hali ya virusi vya corona kwenye eneo au mji unaoishi. Kama utaweza kuwapigia kabla hujaenda, itawasaidia kukuelekeza haraka ni sehemu ipi sahihi unayoweza kwenda kutokana na tatizo lako.Hii pia itakusaidia wewe binafsi na pia itasaidia kuzuia kusambaza virusi na maambukizi mengine.

 

Hakikisha unafuatilia taarifa na fuata ushauri unaotolewa na watalaamu wa afya na serikali.

Kwa maelezo zaidi ya kujikinga wewe mwenyewe na kuwakinga wengine dhidi ya virusi vya corona, unaweza kutembelea tovuti ya Shirika la Afya Duniani kwa kubofya Hapa.